Wahudumu wa afya wanaweza kujua kuwa ninatoa mimba?
Ikiwa hautasema kuwa ulitumia tembe za kutoa mimba na haukutumia Misoprostol ukeni hakuna njia yenye watajua au kudhibitisha ulishinikiza utoaji mimba kwa tembe. Mifepristone na Misoprostol haiwezi kugundulika katika damu yako au mkojo wako, kwa hivyo hata kama watafanya majaribio hawawezi kuthibitisha ulitumia tembe hizi.
Ikiwa umechopeka tembe za Misoprostol katika [1] uke wako wanaweza kuona mabaki ya tembe. Ikiwa ulitumia tembe ukeni na unahitaji matibabu jaribu kwa makini kutoa mabaki ya tembe kutoka kwa uke wako kabla ya kwenda katika kituo cha afya.
Ingawa wahudumu wa afya hawawezi kuthibitisha kuwa ulitumia tembe za kuavya mimba pengine kama ulitumia Misoprostol ukeni, watajua ulikuwa mja mzito na pengine watafikiri umepoteza mimba (uaviaji wa kawaida) Utata unaotokana na kupoteza mimba na kuavya mimba unafanana kabisa kwa hivyo hata kama hawajui kama ulitumia tembe za kuavya mimba watakushughulikia vizuri Hauhitaji kufichua kuwa ulitumia tembe za kuavya mimba ikiwa hautaki kufanya hivyo.
[1] Women on Web. Are there other ways to use the Misoprostol? Retrieved from: https://www.womenonweb.org/en/page/985/are-there-other-ways-to-use-the-misoprostol
Kutumia Tembe za Kutoa Mimba FAQs
- Ninaathiriwa na NSAIDs (dawa zisizo na steroid zinazozuia mwili kutumia mbinu za kibaolojia kujikinga) ikimuisha
- Nawezaje kukabili maumivu yanayohusiana na tembe za kutoa mimba?
- Je kama nitatokwa damu zaidi baada ya kutumia tembe za kutoaa mimba?
- Wanawake kwa kawaida hutokwa damu baada ya kutumia dawa za kutoa mimba?
- Nitatokwa damu kwa muda upi baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
- Naweza kunywa pombe wakati wa utaratibu wa utabibu wa kutoa mimba?
- Naweza kumeza tembe za kutoa mimba?
- Naweza kutumia tembe za kutoa mimba kupitia uke
- Naweza kutumia Misoprostol iliyo na Diclofenac
- Naweza kula wakati wa utaratibu wa kutoa mimba kwa tembe?
- Nahitaji kutumia dawa za kuzuia maambukizi ya bakteria wakati wa kutoa mimba?
- Wahudumu wa afya wanaweza kujua kuwa ninatoa mimba?
*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.