Sera ya Faragha

KUHUSU SISI & UPEO WA SERA HII:

safe2choose (Shirika au Sisi) ni shirika lisilo la faida ambalo lina mfumo wa kidijitali kupitia tovuti pamoja na teknolojia zinazohusiana ili kuwezesha watu kutoka sehemu mbalimbali kuweza kufikia taarifa sahihi na zilizowekwa maalum kuhusu chaguo salama la utoaji mimba kwa lengo la kuwezesha kujua ni wapi, lini na nani anafaa kuweza kutoa huduma salama ya utoaji mimba (Mfumo).
Mfumo huu hukusanya taarifa binafsi (PII) zinazoweza kumtambulisha mtumiaji, wafanyakazi wa Shirika, wenye mikataba ya kujitegemea pamoja na watu ambao hutuma maombi ya nafasi hizo (Watumiaji).
Sera hii ya Faragha inafafanua aina za taarifa binafsi(PII) zinazokusanywa pamoja na haki za Watumiaji zinazohusiana na taarifa binafsi(PII) tunayokusanya. Tunamiliki na kudhibiti vipengele vingi vya Mfumo huu lakini ili kuboresha utendaji kazi, baadhi ya vipengele hutolewa na Watoa Huduma Wengine wa Tatu.

Tumeunda na tunafuata Sera hii ya Faragha ili kulinda faragha ya Watumiaji wetu.

MABADILIKO YA SERA HII & ILANI ZA ZIADA ZA FARAGHA

Tunahifadhi haki ya kubadilisha Sera hii ya Faragha katika siku zijazo. Hatutawafahamisha watumiaji kuhusu mabadiliko madogo ambayo hayaathiri maslahi yao ya faragha – kama vile kuimarisha ulinzi wa faragha, kurekebisha makosa ya tahajia na/au kuongeza taarifa zisizo na umuhimu. Ikiwa kutakuwa na mabadiliko yoyote ya nyenzo, tutawajulisha Watumiaji kuhusu hili kupitia barua pepe. Hii ina maana kwamba ikiwa Mtumiaji hajatoa barua pepe iliyo halali, hatutaweza kumtaarifu kuhusu mabadiliko yoyote kwenye Sera hii. Sera hii ya Faragha inaweza kubadilishwa au kuongezwa ikifuatiwa na sisi kuchapisha toleo jipya au notisi za ziada za faragha zitakazotumika kwenye mwingiliano fulani na sisi. Notisi hizi zinaweza kuongezwa katika Sera hii, kuchapishwa kwenye tovuti ya Shirika na/au kutumwa kwa watumiaji kibinafsi.

VIUNGO VYA TOVUTI ZA WAHUSIKA WA TATU

Sera hii ya Faragha haitumiki kwa tovuti zozote za wahusika wa tatu ambazo zinaweza kuunganishwa au kufikiwa kupitia Mfumo wetu. Hatuwajibiki kwa maudhui yoyote, vipengele, utendaji kazi, desturi za faragha za tovuti au huduma zingine zilizounganishwa. Ukusanyaji wa data na desturi za utumiaji wa tovuti yoyote ya wahusika wa tatu iliyounganishwa itasimamiwa na notisi, taarifa au sera ya faragha, sheria na masharti ya matumizi inayotumika na mhusika huyo wa tatu. Tafadhali tunaomba uzisome.

TAARIFA BINAFSI TUNAZOKUSANYA:

Katika Sera hii ya Faragha, kiujumla tunarejelea taarifa zote binafsi zinazoweza kumtambulisha mtumiaji kama “PII”. Tunakusanya PII nyingi tofauti tofauti kutoka na kuhusu Watumiaji, na PII iliyokusanywa inategemea na Mtumiaji pamoja na hali husika. Kwa hivyo, PII inaweza kujumuisha yoyote au yote yafuatayo:

  • Jina.
  • Barua pepe.
  • Nambari ya simu.
  • Anwani ya IP, mtoa huduma ya intaneti, aina ya kivinjari na lugha.
  • Mahali.
  • Majira ya Saa.
  • Lugha zinazotumika.
  • Umri, jinsia, picha binafsi na taarifa zingine za kibinafsi ambazo Watumiaji hutoa.
  • taarifa ambazo Watumiaji hutoa kuhusu afya zao, masuala ya uzazi/mimba, sababu za kutumia Mfumo pamoja na uwezo wao wa kufikia na kulipia huduma za afya ya uzazi.
  • Hali ya ajira na taarifa kuhusu mwajiri.
  • Ushuhuda na ukadiriaji unaotolewa kwenye kipengele chochote cha Mfumo.

JINSI TUNAVYOKUSANYA TAARIFA ZAKO BINAFSI:

Tunaomba ridhaa yako kabla ya kukusanya PII, na kwa kutumia Mfumo wetu, Watumiaji wametoa idhini yao kwenye (1) vigezo na masharti yaliyoainishwa katika Sera hii ya Faragha pamoja na (2) ukusanyaji wetu, matumizi na uhifadhi wa taarifa yoyote wanayotoa kwa Shirika na/au taarifa yoyote ambayo Mfumo hukusanya kutoka kwenye teknolojia wanazotumia kutumia Mfumo.

Kwa maneno mengine, wakati wowote Mtumiaji anapotumia Mfumo, inaweza kukusanya PII kiotomatiki kupiti teknolojia ambayo Mtumiaji anatumia na itakusanya PII yoyote ambayo Mtumiaji hutoa wakati wa mwingiliano wowote na Mfumo.

Tunaweza kutumia mbinu yoyote au zote kati ya zifuatazo kukusanya Taarifa za Kibinafsi:

  • Utoaji wa hiari wa Watumiaji;
  • Mwingiliano wa sehemu yoyote ya Mfumo na Watumiaji ikijumuisha lakini sio lazima kupitia Watoa Huduma wa Tatu; na
  • Majadiliano/muingiliano na Watumiaji.

Tutaendelea kutafuta njia bora na salama za kukusanya PII. Na ikiwa tutafanikiwa kupata njia hizo, tutarekebisha Sera hii ya Faragha ili kujumuisha mabadiliko yoyote.

JINSI TUNAVYOTUMIA TAARIFA ZAKO BINAFSI:

Tunatumia PII tunayokusanya na/au kumiliki kwa njia zifuatazo:

  • Kuwasiliana na Mtumiaji ikiwa ni pamoja na lakini sio tu kukupa taarifa muhimu na zinazohusiana na chaguo zako za afya ya uzazi.
  • Kuchanganua PII yoyote kwa lengo la kuboresha huduma, bidhaa na thamani tunayowasilisha na/au kuwajulisha Watumiaji na watu wengine kuhusu maboresho kama haya pamoja na kutoa taarifa zinazohusiana.
  • Kufanya kazi za kuendesha Mfumo na/au katika hali ya kawaida na uendeshaji wa Shirika.
  • Kufanya utafiti kwa/au na Shirika.
  • Kwa baadhi ya kozi za mafunzo tunazotoa kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na mashirika mengine, tunawapatia mashirika hayo mengine baadhi ya PII tunazokusanya kuhusu wanachama wao wanaoshiriki katika kozi kama hizo zinazotolewa kwa njia ya mtandao.
  • Juhudi za kupata ufadhili wa pesa, ambazo zinaweza kujumuisha kutoa muhtasari wa PII kwa wahusika wanaotoa au zinazoweza kutoa ufadhili kwa Shirika.
  • Kutoa PII kwa watekelezaji sheria, mashirika mengine ya serikali au mamlaka, au wahusika wa tatu kama inavyotakiwa na sheria inayotumika, amri ya mahakama, wito au mchakato wa kisheria unaotolewa kwa Shirika.

Tutachukua hatua zinazofaa na halali ili kuepuka kulazimishwa kufichua PII yako kwa huluki yoyote ya kiserikali au wahusika wa tatu ambao wanataka kuifikia. Hata hivyo, kuna matukio ambapo huluki za serikali na/au wahusika wa tatu wana haki ya kisheria ya kushurutisha huluki kama vile Shirika letu kufichua PII; na katika hali hizi, Shirika letu litalazimika kufuata.

Kuhusu PII iliyokusanywa na/au kuhifadhiwa na Watoa Huduma Wengine wa Tatu wanaoshiriki katika Mfumo, hatudhibiti matumizi yao na/au uhifadhi wa PII yoyote ile.

Kama ilivyofafanuliwa katika kipengele cha Sera hii ya Faragha yenye kichwa cha habari “HAKI YAKO YA KUFIKIA, KUSAHIHISHA, KUDHIBITI NA KUFUTA TAARIFA ZAKO ZA KIBINAFSI”, una uwezo wa kuathiri tunachofanya na PII yako kama ilivyofafanuliwa katika kipengele hicho.

HAKI YAKO YA KUFIKIA, KUSAHIHISHA, KUDHIBITI NA KUFUTA TAARIFA ZAKO BINAFSI:

Watumiaji ambao tunamiliki PII zao wana haki zifuatazo –

  • Kufikia na kupata nakala za PII zao.
  • Kupata maelezo ya jinsi tulivyopata na tumetumia PII zao.
  • Kusahihisha au kufuta PII zao.
  • Kubadilisha jinsi tunavyotumia PII zao.

Ili kutekeleza mojawapo ya haki hizi, ni lazima Watumiaji watupatie barua pepe halali inayoweza kuthibitishwa na wafuate maagizo yaliyoelezwa hapa chini kwenye kipengele cha Sera ya Faragha inayoitwa “JINSI YA KUWASILIANA NASI IKIWA UNA MAOMBI, MAONI NA MASWALI”. Ikiwa Mtumiaji hatatupatia barua pepe iliyo halali yenye kuweza kuthibitishwa, hatutaweza kuwasiliana naye; na hii inatuzuia (1) kutomfahamisha kuhusu mabadiliko ya sera hii na/au masuala yanayohusiana na PII yake na (2) sisi kuthibitisha utambulisho wake ili kuweza kumruhusu mtumiaji kutumia haki yake ya kufikia, kusahihisha, kudhibiti na kufuta PII yake.

SERA NA UTENDAJI WETU WA FARAGHA KWA WATOTO:

Hatukusanyi taarifa zozote kuhusu watumiaji walio chini ya umri wa miaka 13 kwa kufahamu. Hii ni kwa sababu mwingiliano na Mfumo hauhusishi nyenzo na/au taarifa yoyote ambayo inalenga watoto au inaweza kuwaathiri vibaya, hatuthibitishi umri wa watumiaji kwa kujitegemea kutokana na kutumia tovuti na huduma yetu. Hii inamaanisha kuwa tunaweza kukusanya bila kukusudia baadhi ya PII ya mtoto anayetumia Mfumo wetu. Kwa kiwango ambacho Watumiaji hutoa PII kuhusu watu walio na umri wa chini ya miaka 13, Shirika litashughulikia PII kama hiyo kulingana na Sera hii ya Faragha. Ikiwa tutafahamu kuwa tunaingiliana na mtumiaji aliye na umri wa chini ya miaka 13, tutamtaarifu mtumiaji huyo kuwa anahitaji kibali cha mtu mzima ili atumie Mfumo wetu.

SERA NA UTENDAJI WETU JUU YA USALAMA NA UHIFADHI WA DATA:

Ili kulinda PII yako dhidi ya ufichuzi/matumizi yasiyoidhinishwa, tunachukua tahadhari zifuatazo:

Elimu kuhusu Sera hii: Tunawafahamisha wafanyakazi wetu, wawakilishi na Watoa Huduma Wengine wa Tatu kuhusu maelezo ya Sera hii ya Faragha na umuhimu wa kulinda PII tuliyokusanya na tunaimiliki dhidi ya ufichuzi/matumizi yasiyoidhinishwa.

Maboresho ya usalama: Tuko katika harakati za kuimarisha usalama wa PII yako. Kwa sasa tumetekeleza hatua mbalimbali za usalama zilizoundwa ili kuzuia ufichuzi usioidhinishwa na/au matumizi ya PII yako. Baada ya kukamilisha hatua ya kuimarisha usalama, tutasasisha Sera hii ya Faragha. Ikiwa una maswali yoyote tafadhali wasiliana nasi.

Sera ya kuhifadhi data – Sera yetu ya jumla ni kufuta PII zote ndani ya mwaka 1 tangu tarehe iliyokusanywa. Hata hivyo, kwa sababu ya ugumu wa Mfumo wetu, hii inaweza kutofanyika kila wakati. Pia sera yetu ya kuhifadhi data haitumiki kwa PII iliyokusanywa na/au kuhifadhiwa na Watoa Huduma Wengine wa Tatu.

Sera ya usimbaji data – Tunatambua umuhimu wa kusimba kwa njia fiche PII tunayokusanya na tuko katika mchakato wa kurekebisha Mfumo wetu ili PII zote zisimbwe kwa njia fiche wakati zinapokuwa zimehifadhiwa. Hata hivyo, kwa sasa sio PII yote inayosimbwa kwa njia fiche wakati inapokuwa imehifadhiwa. Pia sera yetu ya usimbaji fiche wa data haitumiki kwa PII iliyokusanywa na/au kuhifadhiwa na Watoa Huduma Wengine wa Tatu.

Watoa Huduma Wengine wa Tatu: Hatujawatathmini binafsi Watoa Huduma Wengine wa Tatu ikiwa wametekeleza tahadhari za usalama wanazodai kuwa wanatumia. Tathmini kama hiyo ni gharama sana na inachukua muda mrefu kwa shirika kama letu kukamilisha lakini pia watoa huduma wengine wa tatu wengi wao hawataruhusu kufanya tathmini kama hizi.

UFICHUAJI WETU WA “USIFUATILIE”:

Hatufuatilii watumiaji kwenye tovuti za wahusika wengine wa tatu kwa lengo la kutoa matangazo kwa wahusika wanaolengwa. Kwa hivyo, hatutekelezi mawimbi ya kutofuatilia (DNT).

JINSI YA KUWASILIANA NASI IKIWA UNA MAOMBI, MAONI NA MASWALI:

Ili kuwasiliana nasi ikiwa una maombi, maoni na/au maswali, tafadhali tutumie barua pepe kwenye privacy@safe2choose.org. Kabla ya kufichua PII yoyote au kufanya mabadiliko yoyote kwenye PII, tutatumia barua pepe uliyotupatia ili kuthibitisha utambulisho wa mtu anayetuma ombi. Faragha yako ni muhimu sana kwetu.

Kama inavyoelezwa hapo juu, ikiwa Mtumiaji hatatupatia barua pepe iliyo halali yenye kuweza kuthibitishwa pindi anapowasiliana nasi awali na kutupatia PII, hatuwezi kuthibitisha utambulisho wake; na hii inatuzuia kuruhusu mtu yeyote kutumia haki zozote zinazohusiana na PII iliyo chini yetu.

USASISHAJI WA MWISHO:

Sera hii ya Faragha ilisasishwa Julai, 2024. Tutasasisha Sera hii ya Faragha angalau mara moja kila baada ya miezi 12.