Utoaji mimba kwa njia ya matibabu [1] kwa kawaida hujulikana kama kutoa mimba kwa tembe. Watu wengine pia huita njia hii kama utoaji mimba wa kujisababishia, utoaji mimba utekelezwao-kibinafsi [2] au kutoa mimba kwa kufanya-mwenyewe.
Ikiwa utatumia tembe za kutoa mimba utashuhudia uvujaji damu na msokoto. Dalili ni sawa na kipindi chako cha hedhi au kama unapopoteza mimba. (utoaji mimba kwa njia ya asili).
Kuna njia mbili za kuwa na utoaji mimba kwa tembe: kutumia Mifepristone na Misoprostol au kutumia Misoprostol tu.
Mifepristone
– Mifepristone ni dawa inayozuia mtiririko wa progesterone, ambayo ni homoni inayosaidia uja uzito. Bila progesterone uja uzito hauwezi kua. [3]
– Mifepristone pia hulegeza mlango wa tumbo la uzazi (sehemu ya chini ya tumbo la uzazi) ambayo huzidisha athari ya Misoprostol. [4]
– Mifespristone tu haitoshi kusababisha utoaji mimba, Misoprostol pia inahitajika. [5]
– Kimsingi Mifepristone hutumika kutoa mimba au kupoteza mimba, hivyo kutegemea na sheria and vikwazo, wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kuipata. [6]
Misoprostol
– Misoprostol ni dawa ambayo husababisha tumbo la uzazi kusonga (au kujikunja), na hii inasaidia katika kuondoa mimba pamoja na uvujaji wa damu na msokoto.
– Unaweza kutumia Misoprostol bila Mifepristone, lakini ni bora zaidi kutumia dawa zote pamoja.
– Misoprostol ina matumizi mengine ya matibabu ya kiafya mbali na kutoaji mimba (kutokwa na damu mingi wakazi wa kujifungua mtoto, vidonda vya tumbo na kadhalika), hivyo kwa kawaida inapatikana sana. [7]
Mifepristone na Misoprostol zimeorodheshwa kama dawa muhimu kulingana na Shirika la Afya Duniani na zina kusudiwa kutumiwa kwa utoaji mimba salama. [8]
Ili kujua jinsi ya kutoa mimba kwa njia salama na yenye ufanisi kwa kutumia Misoprostol na Mifepristone bonyeza hapa. Ikiwa unatumia Misoprostol tu bonyeza hapa.
Usalama wa tembe za utoaji mimba na dalili kinzani
Kutoa mimba kwa njia ya matibabu ni salama kwa wanawake wengi. Kunatuhali chache za kiafya zenye dalili kinzani kwa kutumia tembe za kutoa mimba. [9]
Mifepristone haipendekezwi ikiwa :
– Umekuwa ukitumia steroidi ya muda mrefu (kama vile Prednisone au Dexamethasone) Lakini unaweza kutoa mimba kwa Misoprostol tu.
Utoaji mimba kwa kutumia tembe za Mifepristone na Misoprostol haupendekezwi [10]:
– Ukitumia tembe za kuzuia kushikana kwa damu (viyeyusha damu) kama vile Heparin na Warfarin,
– Ikiwa una kasoro ya kuvuja damu kama vile Porphyria,
– ikiwa una tezi ya adrenal isiyofanya kazi kila mara
– Ikiwa unaathiriwa na Mifepristone, Misoprostol au prostaglandini, utoaji mimba kwa tembe haukupendekezwi kwako. Njia pekee ya kujua kama una unaathiriwa ni ikiwa umetumia tembe hizi awali na ukaathirika. Haiwezekani kujua kama utaathirika au hautaathirika kabla ya kutumia tembe hizi.
– Ikiwa una uja uzito nje ya tumbo la uzazi (nje ya tumbo la uzazi) tembe za kutoa mimba haziwezi kukudhuru, lakini hazitatamatisha uja uzito. Ikiwa unajua una uja uzito nje ya tumbo la uzazi, unahitaji kutafuta msaada wa kiafya mara moja ili kukabili uja uzito nje ya tumbo la uzazi kwa njia salama.
Ikiwa una IUD (kifaa kati-uterasi) si dalili kinzani kwa kutumia tembe za kutoa mimba, lakini inahitaji umakinifu. Hatari ya kuwa na uja uzito nje ya tumbo la uzazi (uja uzito usio ndani ya uterasi) unaongezeka unapokuwa na IUD. Kila mara inapowezekana, pendekezo salama ni kutolewa IUD kabla ya kutumia tembe za kutoa mimba. [11]
Ikiwa huna hakika kama tembe za kutoa mimba ni salama kwako, wasiliana nasi! Tunaweza kukusaidia kujua kama njia hii inakufaa.
Kumbuka safe2choose ina mafunzo tu kusaidia wanawake ambao watatumia tembe za kutoa mimba katika wiki kumi na moja za kwanza za uja uzito. Ikiwa mimba yako imekua zaidi, tutafanya kila tuwezalo kukuelekeza kwa shirika lililojiandaa zaidi kukusaidia. [12]
Cha kutarajia unapotoa mimba kwa tembe
Baada ya kutumia tembe za kutoa mimba utakuwa na dalili zinazofanana na za hedhi au kupoteza mimba. Ikiwa unatumia Mifepristone, hii dawa kwa kawaida haisababishi dalili zozote. Dalili nyingi zitatokea tu baada ya kutumia Misoprostol.
Dalili zinazotarajiwa kutokea zinajumuisha: msokoto, kuvuja damu na pengine kupitisha damu iliyokolea. Kwa kawaida uvujaji damu zaidi na msokoto utatokea katika saa arubaini na nane za kwanza baada ya kutumia Misoprostol, lakini unaweza kushuhudia kuvuja au kutovuja damu kwa siku kadhaa au majuma. [13]
Misoprostol inaweza sababisha madhara ya muda kama vile joto, kibaridi, kuhara, kichefuchefu, kutapika, na kuumwa kichwa. Iwapo hautashuhudia ni kawaida kabisa. Iwapo utashuhudia, zitatoweka baada ya saa arubaini na nane zijazo au chini. [13]
Wasiliana nasi ili kujua namna ya kukabiliana na madhara.
Namna ya kujua ikiwa tembe zilifanya kazi
Ikiwa ulitumia dawa kulingana na maelekezo yaliyopendekezwa, na una uvuja damu nyingi kama unapokuwa na hedhi (au zaidi) kwa saa kadhaa, kuna uwezekano kuwa utoaji mimba kwa matibabi ulifanikiwa. Dalili zako za uja uzito (matiti nyororo, kichefuchefu, uchovu), polepole zinastahili kuimarika na baadaye kutoweka takriban siku tano baada ya kutumia tembe za kuavya mimba. Hii ni dalili nyingine nzuri kuwa tembe zilifanikiwa. [11]
Ingawa si lazima, ikiwa unapendelea kuthibitisha zaidi unaweza kufanya mojawapo ya majaribio haya:
– Jaribio la mkojo (mkojo hcg): Hili ni jaribio rahisi linaloweza kufanywa kwa kuthibitisha, pia linaweza kufanywa faraghani katika nyumba yako. Inapendekezwa kusubiri takriban wiki nne baada ya kutumia tembe za kutoa mimba. Ikiwa mchakato ulifanikiwa, jaribio linastahili kuwa hasi baada ya wiki nne.
– Jaribio la damu (Ujumuishaji hcg): Jaribio hili linahitaji safari ya kimatibabu, na ni bora zaidi ikiwa jaribio la damu hii lilifanywa kabla ya kutumia tembe za kutoa mimba kwa ajili ya kulinganisha viwango vya homoni. Jaribio hili halifanywi kila mara, na hivyobasi kama utapendelea kuthibitisha jaribio la mkojo kama lilivyoelezwa hapo juu hupendekezwa zaidi. Ikiwa utachagua kufanya kipimo hiki, homini ya ujaizito inapaswa kiwa haipo Kwa takriban wiki nne baada ya matumizi ya dawa ikiwa mchakato ulifanikiwa.
– Jaribio la mawimbi sauti: Hii inahitaji safari ya kimatibabu, na inaweza kutumika kubaini mimba inayokua. Kumbuka kuwa kama tembe za kutoa mimba zilifanya kazi, kunaweza kukawa na damu bado na vijinyama vinavyoonekana katika jaribio la mawimbi sauti kwatakriban wiki mbili. Hata kama mimba imetoka, wakati mwingine jaribio la mawimbi sauti hufanywa.
Iwapo saa arubaini na nane zimepita baada ya kutumia kipimo cha mwisho cha Misoprostol na hujavuja damu au kiwango cha uvujaji wako ni chini ya hedhi yako, kuna uwezekano kwamba utoaji mimba haukufanikiwa. [14]
Katika hali nyingi, inawezekana kujaribu tena kwa tembe za kutoa mimba. Wasiliana nasi iwapo hii ni hali yako ili tukupe msaada.
Utunzaji wa kiafya baada ya tembe za kutoa mimba
Iwapo dalili zako ziko zilivyotarajiwa na hauna dalili zozote za kutahadharisha, hauhitaji utunzaji wa kiafya. Si lazima kufanya jaribio la uja uzito au jaribio la mawimbi sauti baadaye, ama kuwa na upasuaji kama vile D&C
Uwezo wa kupata uja uzito na hedhi baada ya kutoa mimba
Baada ya kutoa mimba (kwa upasuaji au matibabu), kipindi cha hedhi yako kitaanza tena, kama kwamba ulikuwa na muda wako wa hedhi. Bado mayai ya kike yataachiliwa tena takriban siku kumi baadaye. Hii inamaanisha kuwa unaweza kuwa na uja uzito tena ikiwa utajamiiana bila kinga. [11]
Ikiwa hauko tayari kuwa mjamzito tena, unapaswa kuzingatia njia za kuzuia mimba. Unaweza kupata habari zaidi kwa FindMyMethod.org
Hedhi yako itakayofuata inaweza kurejea baada ya wiki nne au sita baada ya kutumia tembe za kutoa mimba. [15]
Shirikisho la Uavyji wa Mimba la Kitaifa ni Chama (NAF) safe2choose cha wataalamu wahudumu wa Afya wa kuavya mimba Amerika kaskazini.
Shirikisho la Uavyji wa Mimba la Kitaifa ni Chama (NAF) cha wataalamu wahudumu wa Afya wa kuavya mimba Amerika kaskazini.
carafem hutoa huduma bora na ya kitaalam ya uavyaji wa mimba na upangaji wa uzazi ili watu waweze kudhibiti idadi na nafasi za watoto wao.
[1] World Health Organization. Safe abortion: technical and policy guidance for health systems. Imechukuliwa kutoka: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/;jsessionid=B7AEEBE4F34809D869F73B1ABA7F6221?sequence=1
[2] Reproductive Health Matters. Self-management of medical abortion: a qualitative evidence synthesis. Imechukuliwa kutoka: https://www.tandfonline.com/doi/pdf/10.1016/j.rhm.2016.06.008?needAccess=true
[3] Children by Choice. Medication abortion. Imechukuliwa kutoka: https://www.childrenbychoice.org.au/information-support/abortion/medication-abortion-2/
[4] S. Hopkins MD, M. Fleseriu MD. Chapter 7 – Medical Treatment of Cushing’s Disease. Imechukuliwa kutoka: https://www.sciencedirect.com/science/article/pii/B9780128043400000073
[5] Thoai D Ngo, Min Hae Park, Haleema Shakur & Caroline Free. Comparative effectiveness, safety and acceptability of medical abortion at home and in a clinic: a systematic review. Imechukuliwa kutoka: https://www.who.int/bulletin/volumes/89/5/10-084046/en/
[6] Brooke Ronald Johnson, Vinod Mishra, Antonella Francheska Lavelanet, Rajat Khosla & Bela Ganatra. A global database of abortion laws, policies, health standards and guidelinesArticle has an altmetric score of 221. Imechukuliwa kutoka: https://www.who.int/bulletin/volumes/95/7/17-197442/en/
[7] Webmd. Misoprostol. Imechukuliwa kutoka: https://www.webmd.com/drugs/2/drug-6111/misoprostol-oral/details
[8] WHO. Access to essential medicines as part of the right to health. Imechukuliwa kutoka: https://www.who.int/medicines/areas/human_rights/en/
[9] Ipas. Medical abortion contraindications and precautions. Imechukuliwa kutoka: https://www.ipas.org/clinical-updates/general/ma-precautions
[10] WHO. Essential Medicines List Application Mifepristone–Misoprostol for Medical Abortion. Imechukuliwa kutoka: https://www.who.int/selection_medicines/committees/expert/22/applications/s22.1_mifepristone-misoprostol.pdf?ua=1
[11] Ipas. (2019). Clinical Updates in Reproductive Health. L. Castleman & N. Kapp (Eds.). Chapel Hill, NC: Ipas. Imechukuliwa kutoka: https://ipas.azureedge.net/files/CURHE19-april-ClinicalUpdatesInReproductiveHealth.pdf
[12] National Abortion Federation. 2020 Clinical Policy Guidelines for Abortion Care. Imechukuliwa kutoka: https://5aa1b2xfmfh2e2mk03kk8rsx-wpengine.netdna-ssl.com/wp-content/uploads/2020_cpgs_final.pdf
[13] Planned Parenthood. How does the abortion pill work? Imechukuliwa kutoka: https://www.plannedparenthood.org/learn/abortion/the-abortion-pill/how-does-the-abortion-pill-work
[14] Gynuity. Abortion with self-administered misoprostol. Imechukuliwa kutoka: https://gynuity.org/assets/resources/polbrf_misoprostol_selfguide_en.pdf
[15] BPAS. Caring for yourself after your abortion. Imechukuliwa kutoka: https://www.bpas.org/abortion-care/abortion-aftercare