Kutoa mimba kwa kutumia Misoprostol tu

Utoaji mimba na Itifaki ya Misoprostol

Mimba ya matibabu inaweza kufanywa na Mifepristone na Misoprostol mfululizo au kwa Misoprostol peke yake. Ukurasa huu unaelezea habari juu ya matumizi ya Misoprostol pekee kwa utoaji wa mimba kwa kutumia tembe. Ikiwa tu unaweza kufikia Mifepristone, tafadhali tazama mwongozo huu.

Kabla ya kuanza

Kutumia Misoprostol ni bora sana (80-85%) [1, 2] kumaliza ujauzito ambao ni wiki 13 au chini.

Kumbuka habari hii ni muhimu kwa utoaji mimba kwa tembe za kutoa mimba katika mimba zilizo wiki kumi na tatu au chini zinazohesabiwa [1,2,3] kutoka siku ya kwanza ya kipindi chako cha mwisho wa hedhi yako. Kwa kuwa hatujapewa mafunzo ya kusaidia kutoa mimba zilizo zaidi ya wiki kumi na moja, tutafanya kila tuwezalo kukuelekeza kwa shirika lililo na uwezo wa kufanya hivyo

Ili kuthibitisha kuwa mbinu hii ni salama kwako, tunapendekeza usome kitengo kilichopita kuhusu dalili kinzani kwa kutumia tembe za kutoa mimba. Ikiwa hauna hakika kama utaratibu huu ni bora kwako, wasiliana nasi.

Kipimo cha Misoprostol

Utahitaji Tembe 12 za Misoprostol.

Ikiwa ni ngumu kupata tembe 12, unaweza kuchagua kuendelea na tembe 8 za Misoprostol, lakini ufanisi utapungua, na unapaswa kuwasiliana na washauri wetu.
Ikiwa una ujauzito kati ya wiki 10-13, inashauriwa sana kutumia tembe 12 za Misoprostol.

Kila tembe inastahili iwe 200mcg. [7]

Ikiwa tembe unazozipata ziko katika vipimo tofauti vya mcg, utahitaji kufanya hesabu tena ya jumla ya tembe ili uweze kutumia kipimo kinachofaa cha dawa. [8]

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali usisite kuwasiliana nasi. Tuko hapa kukusaidia katika mchakato wako wote wa kutoa mimba.

Jinsi ya kutumia Misoprostol kwa utoaji mimba salama

Dalili nyingi zitaanza muda mfupi baada ya kutumia Misoprostol, kwa hivyo chagua wakati unaofaa kwako na ratiba yako unapokuwa nyumbani bila majukumu.

Hatua ya kwanza: Meza 800mg ya Ibruprofen

Hatua hii haihitajiki, lakini tunaipendekeza sana. Ibuprofen itapunguza kiasi cha msokoto na kukusaidia kudhibiti uwezekano wa madhara ya Misoprostol [9]. Kumbuka, Ibuprofen inaweza kutumika katika utaratibu wote na baada inapohitajika. Wanawake wanaoathirika na Ibuprofen au NSAIDs wanaweza kushauri ukurasa wa FAQs kwa mapendekezo kuhusu njia mbadala za kukabili maumivu.

Ikiwa una dawa ya kuzuia kichefuchefu, unaweza kuitumia katika wakati huu.

Subiri saa 1


Hatua ya pili: Weka Misoprostol nne chini ya ulimi wako kwa dakika thelathini.

Ni muhimu sana kuwa tembe zisalie chini ya ulimi wako kwa dakika thelathini ili kuziruhusu kuchukuliwa na mfumo wako. Baada ya dakika thelathini unaweza kunywa maji kuosha na kumeza mabaki yoyote ya tembe. [1]

Ikiwa utatapika dakika thelathini Misoprostol inapokuwa chini ya ulimi wako, kuna uwezekano kuwa hazitafanya kazi. Katika hali hii, ni lazima kurudia hatua ya pili mara moja.

Ikiwa utatapika baada ya kuwa na tembe chini ya ulimi wako kwa dakika thelathini, hakuna haja ya kurudia hatua ya pili kwani tembe zitakuwa tayari zimechukuliwa katika mfumo wako.

Subiri saa tatu


Hatua ya tatu: Rudia hatua ya 2 na weka tembe zingine nne za Misoprostol chini ya ulimi wako kwa dakika thelathini.

Subiri saa tatu


Hatua ya nne:Rudia hatua ya 2 na weka tembe zingine nne za Misoprostol chini ya ulimi wako kwa dakika thelathini.

Damu kawaida huanza ndani ya masaa kadhaa. Ikiwa masaa 24 imepita tangu utumie tembe zako 4 za kwanza za Misoprostol na bado huna kutokwa na damu au kubana, wasiliana nasi. Usitumie tembe zaidi hadi tuweze kutathmini hali hiyo pamoja.

Dalili zinazotarajiwa baada ya kutumia Misoprostol kwa kutoa mimba.

Baada ya kutumia Misoprostol utashuhudia msokoto na kuvuja damu. Baadhi ya wanawake (si wote) watatoa damu iliyokolea. Haiwezekani kujua haswa wakati kukandamiza na kutokwa na damu kutaanza, mara nyingi ni ndani ya masaa 24 ya kwanza ya kipimo cha kwanza cha Misoprostol, lakini inaweza kuwa masaa kadhaa baadaye. [10]

Uvujaji damu unaotarajiwa unastahili kuwa mzito kuliko hedhi yako, au angalau ufanane. Unaweza kuwa na utokaji damu au kutotokwa damu kwa siku au wiki kadhaa baada ya kutumia tembe. Dalili zako za uvujaji damu na uja uzito zinastahili kuimarika polepole katika wiki chache zijazo.[11]

Kwa wanawake walio kati ya wiki kumi hadi kumi na tatu, mtakuwa na dalili za kuvuja damu au msokoto, hata hivyo unaweza kuona kijusi kinapopita [1]. Kwa kawaida kijusi hiki huwa kimechanganyika na damu na damu iliyokolea, na mara nyingi kinapita bila kuonekana, lakini ni muhimu kujua kuwa ni kawaida ikiwa utakiona. Usitie shaka, kinaweza kutupwa kwa kikunja kwa visodo au kusukumwa na maji kwa choo.

Kumbuka kuwa kila tukio la kutoa mimba ni tofauti na dalili zinaweza kutofautiana kutoka mwanamke hadi mwanamke.

Wengi wa wanawake ambao wana dalili za uja uzito wanaacha kuwa nazo siku tatno baada ya kutumia Misoprostol. Ikiwa dalili zako za uja uzito zimeanza kupungua na kupotea baada ya kutumia tembe za kutoa mimba, hii ni ishara nzuri kuwa hauna uja uzito tena. [12]

Madhara ya Misoprostol

Baada ya kutumia Misoprostol, wanawake wengine hushuhudia madhara ambayo yanaweza kudumu kwa saa chache [11]. Madhara haya ya Misoprostol ni pamoja na:

  • Joto
  • kuendesha
  • kichefuchefu / kutapika
  • Kuumwa kichwa
  • kibaridi
madhara_wakati-_kutoa_mimba_kwa_kutumia_tembe_za_kutumia_misoprostol_pekee

Tahadhari

Ili kuepuka kuvuja damu zaidi na / au maambukizi, ni muhimu kwa wiki zinazofuata, au hadi uvujaji damu wako upungue [14], uchukue tahadhari zifuatazo.

  • Kutumia pedi kunapendekezwa kufuatilia kutokwa na damu kwako wakati wa siku chache za kwanza za uavyaji mimba, lakini unaweza kubadili kutumia tamponi au kikombe mara tu unapopata raha.
  • Rudi kwenye shughuli zako za kawaida (mazoezi, kazi, n.k.) mara tu unapohisi kuwa tayari.
  • Unaweza kufanya ngono wakati wowote uko tayari; muhimu zaidi ni kusikiliza mwili wako na tamaa.
  • Tafadhali fahamu kuwa unaweza kupata mimba tena muda mfupi tu baada ya kutoa mimba, ndani ya wiki mbili tu.
tahadhari-kuchukua-baada-ya-utoaji-mimba-kwa-tembe

Ishara za onyo: kutafuta msaada

Ikiwa una mojawapo ya dalili zifuatazo, hii inachukuliwa kuwa ishara ya onyo kuwa unaweza kuwa na utata na unapaswa kutafuta matibabu mara moja.

Ukijaza pedi mbili au zaidi (ijae kabisa mbele hadi nyuma, upande kwa upande) katika saa moja au chini na idumu kwa saa mbili mfululizo au zaidi.

  • Joto la nyuzi thelathini na nane ya Celsius za digrii (100.4 digrii Fahrenheit) ambayo haipungui baada ya kumeza Ibuprofen. Mara kwa mara thibitisha kwa kipima joto.
  • Joto la nyuzi thelathini na nane Celsius za digrii (100.4 digrii Fahrenheit) ambayo haipungui saa ishirini na nne baada ya kutumia Misoprostol. Mara kwa mara thibitisha kwa kipima joto.
  • Maumivu ambayo hayapungui baada ya kutumia Ibuprofen.
  • Rangi au harufu ya damu yako ni tofauti sana na kipindi chako cha kawaida cha hedhi au ina harufu mbaya.
  • Ikiwa una wekundu, unahisi kujikuna au mikono inavimba, shingo na uso, inawezekana kuwa una athari ya matumizi ya dawa. Unaweza kutumia antihistamine, lakini ikiwa unapata ugumu kupumua basi athari ya dawa ni mbaya na unahitaji utunzaji wa kimatibabu mara moja. [15]
tahadhari-kuchukua-baada-ya-utoaji-mimba-kwa-tembe

Waandishi:

na timu safe2choose na wataalam wanaounga mkono kwenye carafem, kulingana na mapendekezo ya 2019 na Ipas, na mapendekezo ya 2012 na Shirika la Afya Duniani.

carafem hutoa utunzaji rahisi na wa kitaalam wa utoaji mimba na uzazi wa mpango ili watu waweze kudhibiti idadi na nafasi ya watoto wao.

Ipas ndio shirika pekee la kimataifa linalolenga tu kupanua ufikiaji wa utoaji mimba salama na utunzaji wa mpango wa uzazi.

Shirika ya Afya Duniana ni wakala maalum wa Umoja wa Mataifa unaohusika na afya ya umma ya kimataifa.

[1] World Health Organization. Safe abortion: technical and policy guidance for health systems. Retrieved from: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/;jsessionid=AB2B02D2E41FB4F6CF95B5F59B0A9AF4?sequence=1

[2] Ipas. (2020). Clinical Updates in Reproductive Health. L. Castleman & N. Kapp (Eds.). Chapel Hill, NC: Ipas. Retrieved from: https://www.ipas.org/wp-content/uploads/2020/08/ClinicalUpdatesInReproductiveHealthCURHE20-English-digital.pdf

[3] World Health Organization. Clinical guidelines for safe abortion. 2014. Retrieved from: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/97415/9789241548717_eng.pdf?sequence=1

[4] National Abortion Federation. 2020 Clinical Policy Guidelines for Abortion Care. Retrieved from: https://5aa1b2xfmfh2e2mk03kk8rsx-wpengine.netdna-ssl.com/wp-content/uploads/2020_cpgs_final.pdf

[5] Guttmacher institute. Early Pregnancy Failure: Misoprostol May Be Good Alternative to Surgery. Retrieved from: https://www.guttmacher.org/journals/psrh/2006/early-pregnancy-failure-misoprostol-may-be-good-alternative-surgery

[6] Platais I, Tsereteli T, Grebennikova G, Lotarevich T, Winikoff B. Prospective study of home use of mifepristone and misoprostol for medical abortion up to 10 weeks of pregnancy in Kazakhstan. Retrieved from: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/?term=Prospective+study+of+home+use+of+mifepristone+and+misoprostol+for+medical+abortion+up+to+10+weeks+of+pregnancy+in+Kazakhstan

[7] Gynuity. Efficacy of Misoprostol Alone for First-Trimester Medical Abortion: A Systematic Review. Retrieved from: https://gynuity.org/resources/efficacy-of-misoprostol-alone-for-first-trimester-medical-abortion-a-systematic-review

[8] Elizabeth G. Raymond, Caitlin Shannon, Mark A, Weaver, Beverly Winikoff. First-trimester medical abortion with mifepristone 200 mg and misoprostol: a systematic review. Retrieved from: https://www.contraceptionjournal.org/article/S0010-7824(12)00643-9/fulltext

[9] Livshits, Anna et al. Fertility and Sterility, Volume 91, Issue 5, 1877 – 1880. Ibuprofen and paracetamol for pain relief during medical abortion: a double-blind randomized controlled study. Retrieved from: https://www.fertstert.org/article/S0015-0282(08)00176-3/fulltext

[10] Gynuity. providing medical abortion in low-resource settings: an introductory guidebook. Second Edition. Retrieved from: https://gynuity.org/assets/resources/clinguide_maguide2nd_edition_en.pdf

[11] Planned Parenthood. How does the abortion pill work? Retrieved from: https://www.plannedparenthood.org/learn/abortion/the-abortion-pill/how-does-the-abortion-pill-work

[12] Gynuity. Self-Assessment of Medical Abortion Outcome using Symptoms and Home Pregnancy Testing. Retrieved from: https://gynuity.org/resources/self-assessment-of-medical-abortion-outcome-using-symptoms-and-home-pregnan

[13] National Abortion Federation. Expected Side Effects of Medical Abortion. Retrieved from: https://prochoice.org/patients/using-abortion-pills-on-your-own-what-to-expect/

[14] A.R. Davis, C.M. Robilotto, C.L. Westhoff, S. Forman, J. Zhang. Bleeding patterns after vaginal misoprostol for treatment of early pregnancy failure. Retrieved from: https://academic.oup.com/humrep/article/19/7/1655/2356520

[15] NHS. Risks-Abortion. Retrieved from: https://www.nhs.uk/conditions/abortion/risks/

Chaguzi za Utoaji Mimba Salama kwa kutumia Tembe

huduma zetu