Jinsi ya Kutoa Mimba na Mifepristone na Misoprostol

Utoaji mimba na Itifaki ya Mifepristone na Misoprostol

Mimba ya matibabu inaweza kufanywa na Mifepristone na Misoprostol mfululizo au kwa Misoprostol peke yake. Ukurasa huu unaelezea habari juu ya mchanganyiko wa Mifepristone na Misoprostol kwa utoaji wa mimba kwa kutumia tembe . Ikiwa tu unaweza kufikia Misoprostol, tafadhali tazama mwongozo huu.

Kabla ya kuanza

Kuchanganya Mifepristone na Misoprostol ni mwafaka sana (95%) kutamatisha uja uzito wa wiki 13 au chini.

Kumbuka habari hii ni muhimu kwa utoaji mimba kwa tembe za kutoa mimba kwa mimba zilizo wiki kumi na tatu au chini zikihesabiwa kutoka siku ya kwanza ya kipindi chako cha mwisho cha hedhi. Ikiwa una ujauzito wa zaidi ya wiki 13, mchakato ni tofauti na unahitaji huduma maalum, hivyo tafadhali wasiliana na timu yetu kwa miongozo sahihi na chaguzi zinazopatikana.

Ili kuthibitisha kuwa njia hii ni salama kwako, tunapendekeza usome sehemu ya awali kuhusu dalili kinzani unapotumia tembe za kutoa mimba. Ikiwa huna hakika utaratibu huu ni chaguo nzuri kwako, wasiliana nasi.

Kipimo cha Mifepristone na Misoprostol

Kwa utoaji mimba yenye chini ya wiki 13 utahitaji:
Kidonge kimoja cha 200 mg cha Mifepristone, na

Angalau vidonge vinne vyaa 200 mcg vya Misoprostol.

Hata hivyo, ni bora kuwa na dozi ya ziada ya vidonge vinne vya Misoprostol (800 mcg zaidi), sawa na jumla ya vidonge nane vya Misoprostol (1600 mcg), kwa sababu unaweza kuhitaji kumeza vyote ili kuhakikisha kuwa utoaji mimba umekamilika, hususa ni endapo una ujauzito wa wiki 9-13.

Ikiwa una vidonge vinne tu vya Misoprostol, bado unaweza kuvitumia.

Ni vema Kufahamu kuwa: 200 mg ya Mifepristone na 200 mcg ya Misoprostol ndizo dozi za kawaida, lakini ikiwa vidonge ulivyonavyo vina vipimo tofauti vya mg na/au mcg itabidi uhesabu upya jumla ya vidonge ili utumie kiasi sahihi cha dawa.

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali usisite kuwasiliana nasi. Tuko hapa kukusaidia katika mchakato wako wote wa uaviaji mimba.

Jinsi ya kutumia Mifepristone na Misoprostol kwa utoaji mimba salama

Itifaki ya Utoaji Mimba wa Kitabibu kwa Kutumia Mifepristone na Misoprostol (Chini ya Ulimi) Infografiki

Hatua ya 1: Tumia kidonge cha Mifepristone na maji

Kunywa kidonge kimoja cha Mifepristone cha 200 mg pamoja na bilauri moja ya maji.

Ikiwa uta tapika ndani ya dakika 30 za kwanza baada ya kutumia Mifepristone, dawa inaweza isifanye kazi. Hivyo kama una kidonge cha ziada cha Mifepristone, unapaswa kurudia Hatua ya1.

Subiri kwa saa 24 hadi 48

Subiri kwa saa 24 hadi 48 kabla ya kuendelea na hatua inayofuata. Chagua muda wowote ndani ya kipindi hicho ambapo utaweza kuoga kisha kukaa mahali salama kwa uhuru kwa angalau saa 12 (au saa 24 kwa matokeo bora zaidi) kwani dalili za mimba kutoka zitaanza kuonekana muda mfupi baada ya kutumia Misoprostol.


Hatua 2: Tumia mg 800 za ibuprofen

Kunywa dawa ya kutuliza maumivu kama ibuprofen (mg 800) dakika 30 kabla ya kutumia Misoprostol. Pia waweza tumia Acetaminophen au paracetamol (mg 1000) ingawa huenda zisifanye kazi vizuri kama ibuprofen.

Hatua hii si lazima, lakini inashauriwa sana. Ibuprofen itasaidia kupunguza maumivu ya tumbo na kukusaidia kudhibiti maudhi ya Misoprostol.

Angalia ukurasa wa Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs) kwa mapendekezo ya mbadala ya kudhibiti maumivu.

Ikiwa una dawa ya kuzuia kichefuchefu, waweza kuitumia sasa.

Subiri kwa dakika 30

Baaya ya kunywa dawa ya maumivu, subiri kwa dakika 30 kisha tumia vidonge vya Misoprostol.Hii itafanya dawa ya kutuliza maumivu ifanye kazi. Hata hivyo Ibuprofen inaweza kutumika wakati wowote itakapo hitajika baada ya mchakato kuanza.


Hatua 3: Weka vidonge vinne vya Misoprostol chini ya ulimi wako (sublingually) kwa dakika 30

Weka vidonge vinne vya Misoprostol (mcg 200 kila kimoja) chini ya ulimi wako. Ni muhimu sana kuhakikisha kwamba vidonge viko chini ya ulimi kwa dakika 30 ili viweze kufyonzwa na mwili wako. Unaweza kumeza mate yako, lakini usile wala kunywa chochote ndani ya dakika hizi 30.

Baada ya dakika 30, unaweza kunywa maji na kumeza masalia ya vidonge yaliyobaki. Baadhi ya aina za Misoprostol huyeyuka kwa urahisi, wakati nyingine huchelewa kuyeyuka. Lakini usijali, ikiwa hazita yeyuka, hiyo sio shida. Mradi tu uweke vidonge chini ya ulimi kwa dakika 30, vitafyonzwa na vitafanya kazi vizuri.

  • Ikiwa uta tapika chini ya dakika 30 toka uweke vidonge vyua Misoprostol chini ya ulimi, inawezekana visifanye kazi. Katika hali hii, itabidi urudie mara moja Hatua ya 3 kwa dozi mpya ya vidonge vinne vya Misoprostol.
  • Ikiwa utatapika mara baada ya kukaa na vidonge chini ya ulimi kwa dakika 30, hautahitaji kurudia Hatua ya 3 kwani vidonge vitakuwa tayari vimefyonzwa na mwilini mwako.

Misoprostol hutumika tofauti na dawa nyingine na inaweza kutumiwa kwa njia mbalimbali kutoa mimba. Maelekezo haya yatakuonesha jinsi ya kuitumia kwa kuweka vidonge chini ya ulimi (sublingually). Timu yetu inapendekeza njia hii kwa sababu maelekezo yake ni rahisi kufuata, na haiachi athari yoyote. Hakuna kipimo kinachoweza kugundua dawa mwilini mwako endapo utatumia njia hii.

Hata hivyo, unaweza kuchagua njia nyingine kulingana na hali yako. Kwa mujibu wa ushahidi wa kitabibu, kutumia vidonge vya Misoprostol chini ya ulimi (sublingually) katikati ya fizi na shavu (buccally) au kuwekwa kwenye uke (vaginally) huwa na ufanisi unao lingana. Ikiwa unataka kujua kuhusu njia nyingine za kutumia Misoprostol, wasiliana na timu yetu ya ushauri kwa maelekezo au angalia Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs).

Hatua ya 4: Tumia dozi yapili ya Misoprostol endapo itahitajika

Kwa mimba zenye chini ya wiki tisa:

Ikiwa una ujauzito wenye umri wa chini ya wiki tisa, yawezekana usihitaji dozi ya pili ya Misoprostol.

Lakini, ikiwa saa 24 zimepita tangu utumie dozi ya kwanza ya vidonge vinne vya Misoprostol na

  • haujatokwa na damu au,
  • damu inayotoka ni nyepesi kuliko hedhi yako ya kawaida, au
  • una wasiwasi kuwa damu inayotoka ni kidogo sana,

unaweza kurudia Hatua ya 3 na kutumia vidonge vingine vinne vya Misoprostol kwa njia ile ile kama hapo awali.

Kwa mimba zenye kati ya miezi 9 na 13:

Ikiwa una ujauzito wa wiki 9 hadi 13, inashauriwa kutumia dozi ya pili ya vidonge vya Misoprostol. Hii husaidia dawa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na huongeza uwezekano wa kutoa mimba kwa mafanikio.

Subiri kwa saa nne mara baada ya kutumia dozi ya kwanza ya Misoprostol, kisha weka vidonge vinne zaidi vya mcg 200 chini ya ulimi wako. Viweke kwa dakika 30, na ufuate maagizo kama ilivyo katika Hatua ya 3.

Utarajie nini baada ya kutumia Mifepristone na Misoprostol

Mifepristone

Baada ya kutumia Mifepristone, watu wengi hawapati maudhi yoyote; hivyo unaweza kuendelea na shughuli zako za kila siku.

Watu wengine hutokwa na damu kidogo. Hata kama utatokwa na damu, ni muhimu sana kukamilisha hatua zote, ikiwa ni pamoja na kumeza vidonge vya Misoprostol kukamilisha utoaji mimba.

Misoprostol

Unapotumia Misoprostol, utahisi maumivu ya tumbo na kutokwa na damu ambayo inaweza kuanza dakika 30 mara baada ya kumeza vidonge, lakini inaweza kuchukua hadi saa 24 kabla ya kuanza kutoka. Watu wengi huanza kutokwa na damu ndani ya saa nne hadi sita.

Ni kawaida kupata maumivu makali ya tumbo wakati kizazi kinapo jibana ili kutoa mimba. Ili kupunguza maumivu, unaweza kutumia ibuprofen, tumia chupa ya maji ya moto, fanya massage kati ya kitovu na mfupa wa pelvic, au kaa kwenye choo. Endapo utapata kichefuchefu, kunywa vinywaji visivyo na rangi na kula mlo mwepesi au vitafunwa.

Dawa za maumivu zinaweza kutumika wakati wote wa mchakato. Fuata maelekezo, usizidishe dozi, na epuka kutumia aspirin ya kawaida kwani huongeza hatari ya kutokwa na damu.

Damu inayotoka inaweza kuwa sawa au nzito zaidi ile unayoipata katika siku zako za hedhi.

Unaweza kutokwa na mabonge ya damu na tishu, ambazo zinaweza kuwa za ukubwa tofauti kulingana na jinsi ujauzito ulivyokuwa. Katika ujauzito wa awali, hata vibonge vidogo ya damu vinaweza kuashiria kuwa mimba imefanikiwa kutoka.

Kwa mimba ya zaidi ya wiki 10, huenda ukaona au kuhisi yai la uzazi au fetasi inatoka. Hii ni sehemu ya kawaida kabisa ya mchakato. Ikiwa hili litajitokeza, unaweza kuchagua kuiweka kwenye pedi za usafi au kuitupa kwa kuiflush kwenye choo – fanya chochote kitakacho kufaa.

Hali hii ni ya kawaida na ina maana kwamba dawa inafanya kazi. Tunapatikana kutoa msaada ikiwa unahitaji kuzungumza.

Muda wa kutokwa na damu nyingi na ukali wa maumivu ya tumbo hutofautiana kati ya mtu na mtu. Kila uzoefu wa utoaji mimba ni tofauti.

Hakuna tatizo ikiwa damu haitatoka mfululizo (inakata na kutoka tena), pia hali hiyo inaweza kuendelea mpaka kwenye siku zako za hedhi zinazofuata, ambapo mara nyingi hutokea ndani ya wiki nne hadi sita.

Dalili za ujauzito

Baada ya wiki chache, hali ya kutokwa na damu na dalili za ujauzito zinapaswa kupungua pole pole. Kwa watu wengi, dalili za ujauzito kama vile kichefuchefu na kukojoa mara kwa mara hukoma ndani ya siku chache. Mara nyingi maumivu ya matiti ni dalili ya mwisho kutoweka na inaweza kuchukua hadi siku 10 kabla kupungua baada ya kutumia Misoprostol. Ikiwa dalili zako za ujauzito zitaanza kupungua siku chache baada ya kutumia vidonge, ni ishara kwamba utoaji mimba umefanikiwa.

Madhara ya Mifepristone na Misoprostol

Watu wengi hawapati maudhi baada ya kutumia Mifepristone, lakini wengine wanaweza kuhisi kichefuchefu au kutokwa damu kidogo.

Misoprostol inaweza kusababisha

  • kuharisha
  • kichefuchefu
  • kutapika
  • kizunguzungu
  • maumivu ya tumbo
  • maumivu ya kichwa
  • homa; na
  • kutetemeka
Orodha ya athari wakati wa kuatoa mimba kwa kutumia tembe za Mifepristone na Misoprostol

Ishara za onyo: kutafuta msaada

Ni muhimu kuzingatia mwili wako na jinsi unavyohisi wakati wote wa mchakato. Ingawa si kawaida, kuna baadhi ya dalili za hatari ambazo zinahitaji msaada wa kitabibu mara moja.

Tafuta msaada wa matibabu mara moja ikiwa:

  • Kujaza pedi mbili au zaidi (kulowa kabisa kutoka mbele hadi nyuma, na pande zote) ndani ya saa moja au chini ya hapo na hali hiyo kudumu kwa saa mbili mfululizo au zaidi;
  • Kuwa na homa ya 38°C (100.4°F) inayojitokeza saa 24 baada ya kutumia dozi ya mwisho ya Misoprostol na haipungui baada ya kutumia ibuprofen (thibitisha kwa kipimajoto);
  • Kupata maumivu makali ambayo hayapungui baada ya kutumia dawa za maumivu kama ibuprofen;
  • Kujihisi mgonjwa sana au ikiwa rangi na/au harufu ya damu yako ni tofauti na ile ya hedhi yako ya kawaida – damu inaweza kuwa na harufu mbaya na kuwa rangi ya kahawia, giza, au nyekundu angavu, pia ikiwa unatoa majimaji yenye harufu mbaya na rangi nyingine, inaweza kuwa dalili ya maambukizi;
  • Kupata mzio ikiwa ni pamoja na kuwa na ngozi nyekundu, kuwasha, au kuvimba shingo, uso, au mikono – inawezekana unapata mzio kutokana na dawa. Unaweza kutumia antihistamine, lakini kama unapata shida kupumua basi mzio ni mkubwa na unahitaji huduma ya matibabu mara moja.

Kumbuka, ikiwa unahitaji kutafuta matibabu, si lazima useme kwamba ulitumia vidonge vya kutoa mimba kwani vidonge haviwezi kugundulika ikiwa uliweka chini ya ulimi wako.

Orodha ya ishara za onyo wakati wa kutoa mimba na tembe

Tahadhari na Huduma binafsi baada ya kutoa mimba kwa vidonge

Katika wiki zinazofuata baada ya kutoa mimba kwa vidonge, zingatia vidokezo na tahadhari hizi:

  • Tumia pedi ili kuona kiwango cha damu kinacho toka katika siku chache za kwanza za utoaji mimba; kisha unaweza kutumia tampoon au kikombe cha hedhi siku zinazo fuata.
  • Unaweza kurudi kwenye shughuli zako za kawaida (mazoezi, kazi, nk.) mara tu unapohisi uko tayari.
  • Unaweza kufanya ngono wakati wowote unapohisi uko tayari; jambo muhimu ni kusikiliza mwili wako. Nivema kufahamu kwamba unaweza kupata ujauzito baada ya kutoaa mimba – ndani ya wiki mbili tu – hata kama bado unatokwa na damu.
  • Ikiwa unataka kupima ujauzito baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha kama umefanikiwa, fanya kipimo hicho baada ya wiki nne hadi tano. Kufanya kipimo mapema kunaweza kutoa matokeo ya uongo ya positive. Ikiwa kipimo bado ni positive baada ya wiki tano au ikiwa bado una dalili za ujauzito, wasiliana na timu yetu kwa msaada zaidi.
  • Ni kawaida kuwa na hisia tofauti baada ya kutoa mimba. Watu wengine hujisikia vizuri mara moja, na wengine wanahitaji muda zaidi. Ikiwa unahitaji msaada, njia inayoweza kukusaidia ni kueleza hisia zako kwa mtu unaye mwamini.
Tahadhari za Kuchukua Baada ya Kutoa Mimba kwa tembe (Infografiki)

Uandishi

imeandaliwa na timu ya safe2choose pamoja na msaada wa wataalamu toka carafem, kulingana na Miongozo ya Huduma ya Utoaji Mimba ya WHO ya mwaka 2022; Sasisho za Kliniki za Afya ya Uzazi za mwaka 2023 kutoka Ipas na Miongozo ya Sera za Kliniki kwa Huduma ya Utoaji Mimba ya NAF ya mwaka 2024..
safe2choose inaungwa mkono na Bodi ya Ushauri ya Matibabu inayoundwa na wataalamu wakuu wa Afya ya Uzazi na Haki za Uzazi (SRHR).

carafem inatoa huduma za utoaji mimba na uzazi wa mpango kwa njia rahisi na za kitaalamu ili watu waweze kudhibiti idadi na muda wa kupata watoto.

Ipas ni shirika la kimataifa linalolenga kuongeza upatikanaji wa huduma salama za utoaji mimba na kinga ya uzazi.

WHO ni shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Afya ya umma duniani.

NAF ni shirika la kitaalamu nchini Marekani linalounga mkono huduma salama za utoaji mimba zinazozingatia ushahidi na haki za uzazi.

[1] “Mwongozo wa Huduma za Utoaji Mimba.” Shirika la Afya Duniani, 2022, srhr.org/abortioncare/ Imetembelewa Novemba 2024.

[2] Jackson, E. “Masasisho ya Kliniki katika Afya ya Uzazi.” Ipas, 2023, www.ipas.org/wp-content/uploads/2023/09/Ipas-Clinical-Updates-in-Reproductive-Health-CURHE23b.pdf. Imetembelewa Novemba 2024.

[3] “Mwongozo wa Sera za Kliniki.” Shirikisho la Kitaifa la Utoaji Mimba, 2024, prochoice.org/providers/quality-standards/. Imetembelewa Novemba 2024.

Chaguzi za Utoaji Mimba Salama kwa kutumia Tembe

Huduma zetu